Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa za nguvu za kiume zawa dili

57c8bc2a5a776e14330b843f5018d88b Dawa za nguvu za kiume zawa dili

Thu, 4 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAKRIBANI wanaume zaidi ya 100 kwa mwezi kutoka maeneo mbalimbali nchini hununua dawa ya kuongeza nguvu za kiume.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dei Madai, Salma Madai kwenye Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonyesho ya Bidhaa yanayoendelea viwanja vya Posta Kijitonyama mkoani Dar es Salaam.

Amesema kama muuzaji na msambazaji wa dawa za asili, dawa hiyo ya kuongeza nguvu za wanaume inanunuliwa kwa kiasi kikubwa kutokana tatizo hilo kuwa changamoto kubwa kwa jamii.

“Watu wengi wamekuwa ni waathirika wa nguvu za kiume, ndio maana kati ya bidhaa nilizonazo hii ya nguvu za kiume ununuliwa zaidi ya nyingine,” alisema.

Ametaja dawa nyingine alizonazo ambazo zinatengenezwa kwa miti shamba, mimea na mbegu za matunda kuwa ni dawa ya kupunguza unene, dawa ya kuondoa michirizi pamoja na dawa ya kuondoa maumivu.

Amesema utaalamu huo wa dawa asili alisomea katika chuo cha Muhimbili kwa miezi sita na kwa sasa yupo katika mikakati ya kujiongeza zaidi katika elimu hiyo.

Amesema katika maonyesho hayo yupo hapo kwa ajili ya kukutana na wajasiriamali wengine pamoja na kupanua wigo wa wateja na wajasiriamali mbalimbali.

Amesema aliwahi kufanya biashara ya nguo kwa muda mrefu lakini amebadilisha baada ya kuona dawa za mitishamba zinalipa.

Ametoa hofu kwa wana jamii kutoogopa kutumia dawa asili kwa kuhisi zina madhara huku akisisitiza kuwa dawa hizo zinatokana na miti asili.

Naibu Waziri wa Viwanda Exaud Kigahe wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo amesema nchi ina jumla ya viwnda 61,110 ambavyo vimegawanyika katika viwanda vikubwa, vya kati, vidogo na vidogo sana.

Amesema viwanda vingi vidogo na vya kati vinashughulika na uongezaji wa thamani mazao ya k ilimo, uvuvi, mifugo, misitu na maliasili zingine zinazopatikana kwa urahisi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz