Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa za nguvu za kiume zanunuliwa kwa wingi kunusuru ndoa

2e1dd9df7038e68174706187fe855476 Dawa za nguvu za kiume zanunuliwa kwa wingi kunusuru ndoa

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TATIZO la kupungua kwa nguvu za kiume linachangia ndoa nyingi kuwa hatarini hivyo kuwafanya wanaume kutafuta tiba kwa ajili ya kuzinusuru.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Doi Madai, Salma Madai amesema hayo kwenye Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonyesho ya Bidhaa yanayoendelea viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Madai alisema miongoni mwa bidhaa asili anazouza ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume ambayo takribani wanaume zaidi ya 100 kwa mwezi kutoka maeneo mbalimbali huinunua.

“Watu wengi wamekuwa ni waathirika wa nguvu za kiume, ndio maana kati ya bidhaa alizonayo hii inanunuliwa zaidi ya nyingine,” alisema.

Alitaja dawa nyingine alizonazo ambazo zinatengenezwa kwa miti shamba, mimea na mbegu za matunda kuwa ni dawa ya kupunguza unene, dawa ya kuondoa michirizi pamoja na dawa ya kuondoa maumivu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz