Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa za kufubaza  VVU zaadimika

1cb52f2ab96ba556d7066d3b8013d2db.jpeg Dawa za kufubaza  VVU zaadimika

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imekiri kukabiliwa na uhaba wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi (VVU).

Hata hivyo, imeahidi kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi siku chache zijazo.

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amesema kutokana na changamoto hiyo, Shirika la Misaada la Marekani (USAID) limependekeza kutumia kampuni ya kimataifa ya Chemonics kununua na kusambaza dawa hizo nchini kutokana na ukosefu wa uaminifu.

Umoja wa wananchi wa Kenya wanaoishi na VVU wamesema kutokana na uhaba wa dawa hizo maisha yao yapo hatarini.

Wamesema tatizo hilo limesababishwa na mzozo kati ya serikali ya Kenya na USAID.

Kwa mujibu wa wanaharakati, kucheleweshwa kwa dawa hizo ni kutokana na ya serikali ya Kenya kuongeza ushuru kwa misaada, huku USAID likitilia shaka madai ya rushwa yanayohusishwa na Mamlaka ya Taifa ya Vifaa vya Tiba Kenya.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imesema imesuluhisha tatizo hilo na tayari imesambaza dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi katika kauti 31 kati ya 47 na baada ya siku 5 watakuwa na dawa zinazohitajika za watu milioni 1.4 wanaoishi na VVU nchini.

Chanzo: www.habarileo.co.tz