Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa ya wanaotelekeza wazazi wazee yaja

9626 Dawa+pic TZWeb

Thu, 21 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imesema inaandaa sheria ya kuwabana watu ili kila mmoja amtunze mzazi wake ambaye ni mzee.

Hayo yameelezwa leo Juni 20 bungeni na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu, Cesilia Pareso ambaye ametaka kujua ni lini Serikali itaanza kuwalipa wazee wote pensheni kama ilivyoahidi muda mrefu.

“Tunaandaa sheria hiyo mapema sana, tunataka kila Mtanzania ajitahidi kuwatunza na kuwalea wazazi wake, lakini hata ninyi wabunge mtapata baraka ikiwa kila mbunge atachukua mzee mmoja na kuishi naye,” amesema Ummy.

Akijibu swali la msingi la mbunge wa viti maalumu (Chadema), Anna Gidarya, Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile amesema kwa sasa Tanzania inahudumia wazee 500 katika maeneo mbalimbali lakini idadi ya wazee kwa sasa ni kubwa kutokana na maisha ya Watanzania kuwa yameongezeka hadi kufikia umri wa miaka 65.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na watu Wenye Ulemavu, Antony Mavunde ameliambia Bunge kuwa taratibu zote za kuanza kuwalipa wazee wote Tanzania zimeshaandaliwa kama ilivyoainishwa katika Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Chanzo: mwananchi.co.tz