Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa ya matende, mabusha kupambana na mbu wa malaria

58743 Dawa+pic.png

Tue, 21 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tanzania na Msumbiji zimeanza utafiti wa kutumia dawa ya Ivermectin inayotibu mabusha na matende kwa ajili ya kupambana na mbu anayeambukiza malaria.

Kiongozi wa utafiti huo, Dk Issa Lyimo wa Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI), alisema jana kuwa utafanywa kupitia mradi uitwao Bohemia ambao unafadhiliwa na shirika la kupambana na kifua kikuu, malaria na Ukimwi.

Dk Lyimo ambaye pia ni mkuu wa tafiti za kisayansi wa (IHI) alisema mradi huo ni wa miaka minne na umeanza Februari mwaka huu na utakamilika mwaka 2023, lengo likiwa ni kupata uhakika kama dawa hiyo ina uwezo wa kupambana na mbu wa malaria, usalama kwa binadamu anapoitumia na kama inaweza kupambana na wadudu walio juu ya ngozi ya binadamu kama utitiri, kupe na chawa.

“Kikubwa zaidi ni kuangalia pia mtazamo wa wanaofanyiwa utafiti huo, mapokeo yao na kama ina uwezo wa kupambana na vitu nilivyoviainisha.

“Mradi huu umeidhinishiwa Dola 25.3 milioni za Marekani (zaidi ya Sh50 bilioni ) na unashirikisha taasisi kutoka nchi sita zikiwamo Kenya, Msumbiji, Hispania, Uswisi, Marekani na Tanzania,” alisema.

Akifafanua, Dk Mwanga Kakolo kutoka IHI alisema mradi huo utaanzia katika wilaya mbili za Kibiti na Rufiji mkoani Pwani.

Pia Soma

Alisema wameanza na maeneo hayo kwa sababu ni miongoni mwa machache ya Tanzania Bara ambayo yana kiwango cha kati cha maambukizi ya malaria.

Dk Mwanga alisema lengo jingine la utafiti huo ni kupata namna bora ya kupunguza maisha ya mbu na dawa hiyo itatumika kuwakinga binadamu na wanyama.

Chanzo: mwananchi.co.tz