Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa ya NIMR yatoa mwanga wagonjwa wa corona

NIMR Dawa ya NIMR yatoa mwanga wagonjwa wa corona

Mon, 11 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

DAWA ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) yatoa mwanga wa matumaini kwa wagonjwa wa corona.

Dawa hiyo iliyopewa jina la NIMRCAF ambayo inatokana na mchanganyiko wa vyakula; na katika majaribio imeonesha ina uwezo mkubwa wa kudhibiti virusi vya corona.

Akielezea mchanganyiko huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Tiba Asili cha NIMR, Dk Justine Omolo, amesema ni fomula ya tiba lishe, ambayo ina mchanganyiko wa Pilipili kichaa, Tangawizi, Limao na Kitunguu saumu, Asali na Maji.

Amesema kuwa dawa hiyo inasaidia kumpa nafuu mgonjwa wa corona kwa kutibu dalili zinazotokana na ugonjwa huo na tayari imeshaonyesha matokeo chanya.

“Mchanganyiko wa tiba lishe hiyo sio dawa ya corona,lakini inasaidia kumpa nafuu mgonjwa wa corona kwa kuwa inatibu dalili zinazoambatana na ugonjwa huo,” amesema Dk Omolo na kuongezea kuwa;

"Mpaka sasa tiba lishe hiyo imeshaleta matokeo chanya kwa kuwa imesaidia wagonjwa wengi wa corona na kwamba kwa sasa mahitaji yamekuwa ni mengi, tofauti na awali.

“Mwanzo tulikuwa tukitengeneza chupa 1,000 na tumekuwa tukisambaza hospitali kwa wagonjwa kwa siku chupa 120 hadi 200, lakini sasa mahitaji yamekuwa makubwa na imeonyesha matokeo mazuri kwa wagonjwa,”

Amesema kutokana na mafanikio hayo, Serikali imewaongezea vifaa ambapo kuanzia wiki ijayo wataanza kuzalisha chupa 5,000 kwa siku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live