Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa tamu za HIV kuanza kutolewa

30HIV ArticleLarge Dawa tamu za HIV kuanza kutolewa

Wed, 2 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Mashirika ya kutoa msaada yamesema dawa za kupunguza makali ya Virusi vya UKIMWI zenye ladha tamu ya matunda ya ‘strawberry’ kwa ajili ya watoto zitaanza kutolewa katika nchi za Afrika kuanzia mwakani.

Hizo zitakuwa ni dawa za kwanza zenye ladha tamu kukabiliana na VVU kupatikana kwa ajili ya watoto.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watoto Milioni 1.5 kote duniani wanaishi na Virusi vya UKIMWI lakini wanasema ni nusu tu ya idadi hiyo ndio wanaopokea matibabu.

Moja ya kile inachofanya hali kuwa ngumu kwa watoto wadogo kunywa dawa za Virusi vya UKIMWI ni ladha yake chungu.

Wataalamu wa Afya wanasema sasa hatua ya kusaidia kukabiliana na hali hiyo inawadia – dawa zenye ladha tamu zitakuwa muafaka kabisa kwa watoto wenye VVU.

Hatua hiyo inamaanisha hakutakuwa na haja ya kuvunja mara mbili dawa za watu wazima kwa ajili ya watoto.

Katika kipindi cha miaka michache ijayo, nchi za Benin, Kenya, Malawi, Nigeria na Zimbabwe zitaanza kupokea dawa hizo mpya.

“HUYU MTOENI ASIRUDI” MKURUGENZI ALIEMDHARAU WAZIRI MKUU ATUMBULIWA PAPO HAPO

Chanzo: millardayo.com