Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa mpya ya Ukimwi ya Gammora yatoa matumaini

25563 Pic+ukwimi TanzaniaWeb

Tue, 6 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Jerusalem, Israel. Matokeo ya majaribio ya kwanza ya tiba kwa binadamu ya dawa ya virusi vya Ukimwi (VVU), Gammora, yameonyesha kwamba inaweza kuondoa hadi asilimia 99 ya virusi ndani ya wiki nne za matibabu.

Matokeo hayo yaliyotolewa Jumapili yanaonyesha kwamba Gammora imepunguza kwa kiasi kikubwa kwa kuua chembechembe zilizoambukizwa bila kuharibu zenye afya, tofauti na dawa za ARV zinazotumika kufubaza usambaaji wa virusi.

Utafiti huo ulifanywa na watafiti kutoka Taasisi ya Tiba ya Zion Medical ya Chuo Kikuu cha Hebrew cha Yerusalemu, Israel.

"Dawa hiyo huchochea nguvu ya kusababisha seli zilizoambukizwa kujiharibu zenyewe kitendo kinachoitwa kujiangamiza. Ina uwezo wa kutibu wagonjwa walioambukizwa VVU kwa kuharibu seli zote zilizobeba jeni zenye VVU.”

"Matokeo haya ya mwanzo ya majaribio yalikuwa nje ya matarajio yetu na yanaahadi matumaini ya kupata tiba ya ugonjwa huo," Dk Esmira Naftali, mkuu wa maendeleo katika Taasisi ya Tiba ya Zion Medical, alisema, akiongezea kuwa wagonjwa tisa katika Hospitali ya Ronald Bata Memorial nchini Uganda walikuwa wamepewa dozi tofauti ya dawa kwa wiki nne hadi tano.

Katika sehemu ya pili ya majaribio yaliyofanyika wiki mbili baadaye, wagonjwa walipewa dawa na matibabu ya ziada ya kinga baada ya wiki nne hadi tano.

Wagonjwa walipewa dawa za kinga aina lopinavir 800 mg na ritonavir 200 mg (LPV + r) kila siku kwa kuchanganya na Gammora mara mbili kwa wiki, au LPV + r tu.

Matokeo yalionyesha kuwa matibabu ya pamoja yaliondoa hadi asilimia 99 ya ujazo wa virusi ndani ya wiki nne bila kuonyesha madhara yoyote.

Wakati wa utafiti wa wiki 10, wagonjwa katika makundi mawili walionyesha ongezeko kubwa la hesabu za seli za T yaani jina lingine kwa seli za CD4, ambazo zina jukumu kubwa katika mfumo wa kinga ya mwili.

Chanzo: mwananchi.co.tz