Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Dawa hizi zinatolewa bure’

Waziri Ummy3c3c3ad0b068 780x470 ‘Dawa hizi zinatolewa bure’

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema dawa myeyuko za Amoxicillin, Zinki na ORS kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano zinatolewa bure na ni marufuku kuuzwa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo leo Mei 12, 2023 bungeni mjini Dodoma.

Amesema dawa hizo zinanunuliwa na serikali kwa kushirikiana na wadau na kusisitiza kuwa dawa hizo haziuzwi zinatolewa bure kwa wananchi.

Amesema katika kipindi cha Julai 2022 hadi Machi 2023, Wizara ilinunua na kusambaza dawa kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) ya kidonge myeyuko cha Amoxicillin vidonge milioni 30.1, na dozi 94,300 za Zinki na ORS kwa ajili ya matibabu ya kuharisha.

“Naomba kutumia fursa hii kusisitiza kwamba dawa za kidonge myeyuko cha Amoxicillin, Zinki na ORS kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, zinanunuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau na dawa hizi hazipaswi kuuzwa,” amesema.

Amewaelekeza waganga wakuu wa mikoa na halmashauri wasimamie suala hilo kwa ukamilifu.

Amesema ununuzi wa dawa hizo uliwezesha kuimarika kwa upatikanaji wa dawa za watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika vituo vya kutolea huduma kwa asilimia 90, ikilinganishwa na asilimia 85.3 katika kipindi hicho mwaka 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live