Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari ataja faida kurekebisha maumbile

Mloganzila Upasuaji Makalio Daktari ataja faida kurekebisha maumbile

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila, Dk Erick Muhumba amesema miongoni mwa faida za upasuaji wa kurekebisha maumbo ni kuepuka magonjwa yasiyoambukiza yanayosababishwa na uzito mkubwa ikiwemo shinikizo la juu la damu, saratani, magonjwa ya figo, magonjwa ya moyo, kiharusi na mengine.

Aidha, alisema wapo watu wanapata msongo wa mawazo kutokana na kutojikubali maumbile yao hivyo watakapofanyiwa upasuaji watajiamini na kuepukana na sonona hivyo kuwa na afya njema.

Dk Muhumba alisema Tanzania imeshaanza kufanya maandalizi kwa ajili ya utalii wa matibabu na kuwa upasuaji huo wa kurekebisha maumbile ni nafasi kubwa ya utalii wa matibabu kwani watu kutoka nchi mbalimbali watafika kufuata huduma hiyo na kuongeza kipato cha nchi.

“Watu walikuwa wanaenda nje ya nchi kwa ajili ya kupata huduma za upasuaji huu wa maumbile na baada ya kuanzisha huduma ya kuweka puto tulikuwa tukiulizwa kwamba kama mtu akikonda sana na nyama kutepeta itakuwaje?

“Kutokana na maswali kama hayo tukaona kuna umuhimu wa kuleta mtaalamu ili huduma ije kufanyika hapa ndani ya nchi na ifanyike kwa gharama nafuu, hivyo huduma hii ni muhimu nchini kwetu pia,” alisisitiza. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live