Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari akemea wanaowafunga kamba wagonjwa Afya ya akili

Brain Daktari akemea wanaowafunga kamba wagonjwa Afya ya akili

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: Nipashe

Dk Babu Meng'oriki amekemea tabia ya baadhi ya watu kuwafunga kamba wagonjwa wa akili kwani sio jambo jema.

Dk.Meng'oriki amekemea tabia hiyo leo Oktoba 6 wakati akizungumza na Nipashe juu ya madhara ambayo yanaweza kutokea kwa mama mwenye tatizo la Afya ya akili mara baada ya kujifungua.

Amesema tatizo hilo linatokea baada ya masaa 48 mpaka wiki mbili au wiki 12 baada ya kujifungua.

Amesema mama mwenye tatizo hilo baada ya muda huo anaweza kupata madhara ya kuwa na msongo wa mawazo, kutelekezwa na mwenza wake na kukosa matunzo na kumfanya aendelee kuandamwa na ugonjwa huku akimuona mtoto kama mzigo.

Mtaalamu huyo wa uzazi amesema mtu mwenye tatizo hilo akifungwa kamba anaweza kupata majeraha na kusababisha tatizo jingine.

Ameyataja madhara kwa mtoto kuwa ni kutupwa na mama, kukosa malezi ya mama na mtoto kukosa maziwa ya mama.

Dk. Meng'oriki amesema mama anapopata tatizo la Afya ya akili wapo ndugu wanaomuacha na mtoto wakisema hawezi kumfanya kitu lakini wanapaswa kuhakikisha mtoto anakuwa salama na mama mwenyewe.

Anasema kila Hospitali au kituo cha Afya wanatakiwa wawepo wataalamu wa Afya ya akili ili mama mjamzito akienda kliniki aweze kupewa elimu juu ya tatizo hilo.

Mtaalamu huyo wa Afya amesema hamna ulazima wa kila mtu anayepatwa na ugonjwa huo kukimbiziwa Hospitali ya Mirembe badala yake apelekwe kituo cha Afya au Hospitali iliyopo karibu ataweza kusaidiwa kwa kuwa dawa zipo za kutosha.

Nipashe imepata nafasi ya kuongea na mkazi wa Babati Neema Paul amesema jamii haina uelewa juu ya tatizo hilo bali ikiona mtu wa namna hiyo inawaza kuwa amerogwa

Chanzo: Nipashe