Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari aeleza saratani ya matiti ilivyo tishio

82327 Pic+saatani Daktari aeleza saratani ya matiti ilivyo tishio

Thu, 31 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Licha ya elimu kuendelea kutolewa kuhusu athari za  saratani ya matiti, idadi ya wanawake wanaougua ugonjwa huo inazidi kuongezeka.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Oktoba 30, 2019 na mkurugenzi wa huduma za kinga ya saratani wa taasisi ya saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa na kubainisha kuwa wagonjwa wamekuwa wakiongezeka ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita.

Amebainisha kuwa hatua zisipochukuliwa inaweza kuleta athari zaidi kwa kuwa umri wa waathirika umezidi kushuka kufikia miaka 52 kutoka 62,  pia wapo wenye miaka 18 hadi 20.

“Hii imesababishwa na mabadiliko ya mfumo wa maisha matumizi ya pombe, tumbaku, unene uliokithiri, vyakula na kutofanya mazoezi,” amesema.

Amesema mwaka 2019 taasisi hiyo imefanya uchunguzi kwa wanawake 1,493 na kati ya hao 370 waligundulika kuwa na uvimbe.

Amesema kati ya wanawake hao,  74  walibainika kuwa wana saratani na tayari wameanzishiwa tiba. Dk Kahesa ameitaja mikoa inayoongoza kwa wagonjwa wengi wa saratani ya matiti kuwa ni Dar es Salaam, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Mwanza.

“Idadi ya wagonjwa waliokuwa wanaonekana kwenye hatua za juu imepungua, awali asilimia 90 ya wagonjwa wa saratani walikuwa wakigundulika katika hatua za juu.”

“Sasa hivi kuna matibabu mazuri, dawa zinapatikana kwa asilimia 91 na mashine za mionzi zipo, wataalamu pia wameongezeka kuhakikisha tunatoa huduma sahihi,” amesema Dk Kahesa.

Chanzo: mwananchi.co.tz