Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari: Nguo za ndani zinazobana hatari kwa afya ya ngozi

Best Cotton Underwear For Women Daktari: Nguo za ndani zinazobana hatari kwa afya ya ngozi

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya magonjwa 3,000 ya ngozi yanatajwa kuathiri watu duniani yakitokana na mfumo wa maisha ya kila siku huku visababishi vikiwa ni vipodozi, vyakula, mavazi na wengine wakirithi magonjwa hayo.

Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake Mtaalamu wa Magonjwa ya Ngozi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, Dk Titto Shengena (Dermatology) amesema kuwa tafiti nyingi zimefanyika na zinaonyesha kuwa nguo za kubana za ndani na zenye rangi nyingi ni hatari kwa afya ya ngozi.

Amesema kuwa wanawake wengi ni waathirika wa magonjwa ya ngozi kwa kuwa wamekuwa wakitumia vipodozi na kuvaa nguo zenye rangi nyingi na za kubana huku wakitumia kwa kiwango kikubwa rotion ambayo ina kemilikali inayotumika kuhifadhia isiharibike ‘lanoline’ nayo inasababisha ngozi kuwasha.

“Unajua ngozi ni urembo ndio maana mtu akipata tatizo la ngozi anaathirika kisaikolojia angalia hata wanaopata chunusi huwa wanahangaika kupaka ‘rotioni’ wakati sio ugonjwa jamii inapaswa kupata elimu sahihi kutoka kwa wataalamu ili wapate ushauri endelevu ili uweze kuwasaidia,” amesema Dk Shengena.

“Upo ugonjwa ambao hujitokeza umri ukiwa mkubwa kuanzia miakai 50 lakini watoto wanapata upele, mapunye ambayo ni fangasi ya nywele pia ugonjwa wa kurihti pumu, mafua nagozi kuwa kavu na kuna wale wanaokula mazao ya bahari mfano samaki wasio kuwa na magamba inakuwa changamoto kwao,” amesema Dk Shengena.

Asha Hussein mkazi wa Mtwara Mjini amesema wanawake tunakuwa wahanga wa magonjwa ya ngozi kutokana na hali hali ya maisha huku wengi wao wakiathiriwa na nguo na vipodozi.

“Wengi tunapenda kuvaa kupendeza ndiyo maana tunavaa nguo za kubana na wakati mwignine tunavaa nguo za ndani zinatuwasha kuna wakati hadi pedi tukivaa zinatuwasha lakini pia kwenye vipodozi ndio hatari zaidi wengi wanameza vidonge wanakuwa kama wazungu wakipata shida kwenye ngozi ni tatizo kubwa kutibu,” amesema Hussein.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndumbwe Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Ally Mshamu anasema kuwa ugonjwa wa ngozi ni hatari husababisha mtu ashindwe kujiamini na wengi huathirika zaidi kwa kuwa wanakuwa na imani potofu.

“Nimeshuhudia mtoto akishindwa kwenda shule na kushindwa kutimiza ndoto zake kutokana na ugonjwa ya ngozi ni hatari kwa kuwa watu wengi hawana uelewa juu ya afya ya ngozi watalaamu wana kazi kubwa ya kutoa elimu,” amesema Mshamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live