Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari: Kula sana hatari mwezi wa Ramadhani

E0c8457768f9cd51f1c8f95adcdd8bb7 Daktari: Kula sana hatari mwezi wa Ramadhani

Thu, 6 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi amesema wakati mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuna ongezeko la tatizo la mshtuko wa moyo kwa sababu ya kula chakula kingi hadi kuvimbiwa.

Katika andiko lake Dk Janabi alieleza kuwa, kila mwaka vifo hivyo vinaongezeka zaidi kipindi hiki cha Ramadhani na wakati wa sherehe zikiwemo Krismasi, Pasaka na mwaka mpya.

Dk Janabi alieleza kwenye andiko hilo kuwa, wanaofunga wafunge kwa kula kiasi hasa vyakula vyenye protini nyingi kuliko wanga hasa kwa wenye matatizo ya moyo ikiwa ni pamoja na kupunguza sukari nyingi.

“Katika mwezi huu wa Ramadhani familia nyingi nchini na duniani kwa jumla raia wake wanafunga, saumu hii tukufu kama nguzo moja kati ya tano za kiislaam. chakula cha jioni au futari mbali ya kuwa na aina mbalimbali za vyakula pia huwa ni vingi kuliko siku za kawaida,” alieleza.

Dk Janabi alieleza kuwa asilimia kubwa ya magonjwa ya moyo yanaweza kuzuilika kwa kuacha kuvuta sigara, kula vyakula bora na kwa kiasi, kupunguza uzito, kufanya mazoezi na kupunguza unywaji wa pombe.

Chanzo: www.habarileo.co.tz