Marekani. Wakati maambukizi ya virusi vya corona vilivyoanzia China vikiendelea kusambaa katika nchi mbalimbali duniani, wataalamu wa afya wanasema kuna baadhi ya watu hawajui hatua za kuchukua endapo wanakuwa na dalili za ugonjwa huo.
Inaelezwa kuwa kumekuwa na mkanganyiko kidogo kwa baadhi ya watu kuhusu hatua gani za kufuata na wapi pa kupimwa na kutibiwa.
Mkurugenzi wa matibabu wa Shirika la Taifa la Magonjwa ya kuambukiza ambaye pia ni profesa katika Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Vanderbilt, Dk William Schaffner, anasema, “kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kujiuliza kwanini unadhani una virusi vya corona?
“Vipi kuhusu mabadiliko ya hali yako, umerudi kutoka nchi fulani na ulisalimiana na mtu kutoka nchi nyingine ambako kuna maambukizi ya virusi vya corona?
Wataalamu hao wanasema kitu cha kukitilia shaka zaidi ni kwamba kama unasumbuliwa na magonjwa ya moyo, kisukari na mapafu, utakuwa katika hatari zaidi ya ugonjwa huo.
Wanasema hata kama hauumwi corona, ila una dalili zote za ugonjwa huo, unapaswa kuwasiliana na daktari kwa ushauri zaidi.
Pia Soma
- Hofu, ulevi chanzo mashabiki Simba, Yanga kuzimia uwanjani
- TikTok yaitetemesha Facebook, Instagram
- Hii ndio roboti ya kupambana na usambaaji wa virusi vya corona China