Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari: Hakuna madhara ya kiafya kwa mama anayenyonyesha kupata chanjo

Ce211668af375e87959b0a7ba274d8d3.jpeg Daktari: Hakuna madhara ya kiafya kwa mama anayenyonyesha kupata chanjo

Sun, 8 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya ndani ya mapafu na maambukizi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Grace Shayo amesema hakuna madhara yoyote ya kiafya kwa mtoto endapo mama anayenyonyesha atapata chanjo ya corona.

Shayo ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), alisema badala yake mama anaponyonyesha mtoto baada ya kupata chanjo inafanya na mtoto kuongeza kinga ya mwili na kuepuka magonjwa.

“Baada ya mama kuchoma chanjo kinachopatikana kwenye maziwa yake ni zile kinga mwili ambazo zimezalishwa na chanjo inayotengenezwa na mwili na sio chanjo, ndio maana tunasisitiza kuwanyonyesha watoto kwasababu maziwa ya mama ni kinga kwa mtoto kupata mgonjwa mbalimbali.”

“Chanjo zitakapotengeza kinga ambayo ni ‘antibody’ itapita kwenye maziwa ya mama ambayo yatamkinga mtoto na maambukizi ya corona kupitia maziwa,” alisema Dk Shayo.

Alisema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kirusi cha corona hakizuii mama kunyonyesha mtoto, hivyo hata kwa chanjo hakuna kizuizi.

“Kwenye covid-19 miongozo ya WHO inashauri mama aendelee kumyonyesha mtoto na azingatie tahadhara zote za kiafya kwasababu hakuna ushahidi wa virusi kupenya kwenye maziwa, hivyo wanashauriwa kujikinga kwa kuvaa barakoa na kunawa mikono wakati wa kumyonyesha mtoto.”

“Wote tunafahamu kuwa kirusi cha Delta pia kinaanza kuathiri wenye umri mdogo kwasababu kipindi kinaanza watu wenye umri mkubwa walipata maambukizi, lakini sasa hata wa umri mdogo wanapata maambukizi,” alisema

Aliwashauri wakinamama kusikiliza zaidi wataalamu wa afya na kupata chanjo hiyo kwa ajili ya faida yao na watoto wao.

“Kina mama wanaonyonyesha natoa wito wajitokeze kupata chanjo kwasababu kwenye maziwa hakuna mwinginliano na chanjo,” alisema Dk Shayo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz