Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DKT JINGU AONYA MALEZI HOLELA KWA WATOTO

24cece8a9a7b941df5016958c0ba5ab3 DKT JINGU AONYA MALEZI HOLELA KWA WATOTO

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii ) Dkt John Jingu ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya malezi kwa watoto wadogo wadogo mchana kurekebisha kasoro zilizopo ili watoto waweze kulelewa katika mazingira sahihi na kwa kujibu wa sheria.

Dkt Jingu ametoa agizo jijini Arusha baada ya kutembelea baadhi ya vituo na kubaini kuwa havizingatii masharti ya utoaji wa hudama kwa watoto wadogo kama ilivyoainishwa kwenye sheria na miongozo.

“Eneo hili halikidhi vigezo na mazingira ya kuwa kituo cha malezi ya watoto mchana kwa hiyo nawapa wiki mbili mrekebishe mapungufu yote, mtafute eneo jingine, maafisa ustawi waje kufanya ukaguzi,baada ya siku 14 kama mtakuwa hamjakidhi tutakifunga,” alisema Dk Jingu.

Alifafanua kuwa huduma ya malezi kwa watoto inapaswa kuzingatia vigezo mbalimbali ikiwemo vyumba vya madarasa, viwanja vya michezo na wahudumu wa kutosha na wenye sifa.

Wizara imepanga kufanya operesheni maalum kwenye vituo hivyo nchi nzima ili kuendana na matakwa ya Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009.

Kwa upande wao baadhi ya wasimamizi wa vituo vilivyokaguliwa wamekiri vituo hivyo kuendeshwa kinyume cha utaratibu ikiwemo kutokuwa usajili pamoja na mazingira yasiyofaa kwa malezi ya watoto wadogo.

Wakati huo huo Katibu Mkuu amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii Jijini Arusha kukagua vituo vya malezi ya watoto mchana mara kwa mara ili kubaini kasoro zikizopo na kuzitafutia ufumbuzi.

Chanzo: habarileo.co.tz