Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chuo cha kairuki kuendelea kusomesha nje

7d8557208fa0dea4f082c1c93dce88d3 Chuo cha kairuki kuendelea kusomesha nje

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHUO cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki (HKMU), kimeendelea na mpango wake wa kufadhili masomo ya wafanyakazi wake kwa ngazi ya uzamili na uzamivu ndani na nje ya nchi.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Makamu Mkuu wa huo hicho, Profesa Charles Mgone wakati wa mahafali ya 18 ya chuo hicho.

Kwenye mahafali hayo, wahitimu 146 walitunukiwa stashahada ya uuguzi, 53 shahada ya uuguzi, 183 shahada ya udaktari wa binadamu na wawili shahada ya uzamivu ya udaktari wa binadamu.

Alisema wahadhiri wanne wamemaliza mafunzo yao ya uzamili hivi karibuni akiwemo Dk Fulgence Mpenda, Dk Jane Nyandele, Dk Hosiana Msechu na Dk Zahra Moraweji.

Profesa Mgone alisema hivi sasa chuo hicho kina wahadhiri 15 wanaosomea shahada ya uzamivu na saba shahada ya uzamili katika fani mbalimbali huku wahadhiri sita wakipandishwa vyeo katika fani mbalimbali.

Alisema katika kuboresha ufundishaji chuo kimeajiri wafanyakazi wapya ili kuendana na ongezeko la wanafunzi na tangu Desemba 2019 mpaka Novemba mwaka huu chuo kimeajiri wafanyakazi wapya nane.

Kuhusu utafiti, Profesa Mgone alisema tafiti mbalimbali zinaendelea kufanywa na wanataaluma wa chuo na wanafunzi wake wa ngazi zote zingine zikihusu magonjwa ya kuambukizwa na yale yasiyo ya kuambukizwa.

Alisema kwa mwaka 2020 baadhi ya wataalamu wa chuo hicho wametoa machapisho kadhaa katika majarida ya kisayansi yakiwemo ya uchambuzi yakinifu kuhusu elimu ya uuguzi na ukunga nchini na utafiti kuhusu njia mpya za kutibu maralia.

Alitaja machapisho mengine kuwa ni uhusiano kati ya ugonjwa wa selimundu na malaria, dalili za mwanzo za kuelekea kupata ugonjwa wa kisukari na aina ya magonjwa yanayowasibu watoto wachanga waliozaliwa kabla ya wakati.

“Kwa niaba ya chuo napenda kuwapongeza wanataaluma na wanafunzi wote kwa hayo machapisho ambayo yametambulika kitaifa na kimataifa,” alisema

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Afya na Elimu la Kairuki, Kokushubila Kairuki aliwapongeza wafanyakazi wote wa chuo hicho kwa namna wanavyozidi kukipandisha hadhi mwaka hadi mwaka kutokana na kila mmoja kuwajibika kwa upande wake.

“Kipekee napenda kumpongeza Profesa Mgone kwa umahiri na ubunifu wake uliohakikisha chuo hiki kinaendelea hata wakati wa janga la korona wakati wenzetu wanafunga vyuo yeye alihakikkisha hapa kila kitu kinakwenda sawa,” alisema

Aidha, aliipongeza Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwa namna ambavyo imekuwa ikitoa mchango wa kuhakikisha chuo kinapata anafunzi kwa kutangaza kozi zake kila yanapotokea maonyesho ya vyuo vikuu yanayoandaliwa na taasisi hiyo kila mwaka.

Chanzo: habarileo.co.tz