Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chuo Kikuu Aga Khan chainadi nafasi ya mwanamke

Chuo Kikuu Aga Khan chainadi nafasi ya mwanamke

Sun, 10 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Chuo kikuu cha Aga Khan kimesisitiza umuhimu wa kuwaelimisha wanawake na kutambua nafasi waliyo nayo kwenye jamii.

Akizungumza  wakati wa  kongamano la kujadili nafasi ya mwanamke, mkuu wa chuo hicho, Profesa Joe Lugalla amesema kuna umuhimu wa kutambua nafasi ya mwanamke katika jamii na kuweka usawa kati ya mwanamke na mwanaume.

"Tumeamua tujadili pamoja nafasi ya mwanamke na kujua mikakati iliyopo ili kutambua umuhimu na nafasi waliyonayo katika jamii," amesema Profesa Lugalla.

Amesema tafiti zinaonyesha kuwa mwanamke akipata nafasi ya elimu na kipato kinachoendana na kazi yake, taifa linaweza kunufaika kutokana na nafasi aliyonayo kwenye jamii.

Mwanzilishi wa Taasisi ya Soma Book Café, Demere Kitunga amesema kuna umuhimu wa kuwahimiza wanawake watakaoandika vitabu kutokana na idadi kubwa ya vitabu kuandikwa na wanaume.

"Maisha tunayopitia idadi ya vitabu vingi vimeandikwa na wanaume, unakuta vinatuelezea hivyo kuna umuhimu wa kuwahimiza wanawake katika nafasi hiyo," amesema Demere.

Mkuu wa kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) chuoni hapo Arbogast Fabiani amesema kuna haja ya kuweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha wanawake kushiriki katika maendeleo ya teknolojia.



Chanzo: mwananchi.co.tz