Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanjo ya saratani haihusiani na uzazi wa mpango

Saratani Agizo Chanjo ya saratani haihusiani na uzazi wa mpango

Fri, 26 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WIZARA ya Afya imesema chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV) imethibitishwa kuwa ni salama hivyo haina madhara kwa watumiaji na kuitaka jamii kutohusisha na uzazi wa mpango.

Chanjo hiyo imeanza kutolewa kwa mabinti wenye umri wa miaka tisa hadi 14 ambapo hadi Disemba ,2024 mabinti milioni 5 wanatarajiwa kupata chanjo hivyo ya dozi mmoja.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo kwa viongozi wa dini ,Meneja mpango wa Taifa wa Chanjo,Dk Florian Tinuga amesema utafiti umeonesha dozi moja ya chanjo hiyo inatoka kinga kamili ya dozi mbili na chanjo hivyo sio mpya.

Amebainisha kuwa wanatoa dozi moja kwasababu tafiti zimeonesha dozi moja inatosha chanjo kamili kama dozi mbili na pia mwangozo wa shirika la afya Duniani (WHO) mwaka 2022 unaruhusu na mapendekezo ya kamati ya kitaalamu kuhusu Maswala ya chanjo Tanzania.

“Saratani ya mlango wa kizazi haina dalili na hivi virusi vya HPV vinakaa kwa mwanaume ambapo wakati wa kujamiiana anahamisha kwa mwanamke hivyo namna ya kujinga ni kupata chanjo,kuepuka ngono katika umri mdogo na kufanya uchunguzi wa kitaalamu ili kugundua dalili za awali na kuwahi kwenya uchunguzi,”amesisitiza.

Dk Tinuga amesema chanjo hiyo sio mpya ambapo walianza majaribio mwaka 2014 mkoani Kilimanjaro na mwana 2018 ikaanza kutolewa bure nchi nzima.

Ameeleza kuwa katika utoaji utaratibu uko katika mifumo minne ambayo ni kufanya kampeni kuwafikia watu wengi, tunafanya mabadiliko ya sera ya chanjo, mfumo wa kawaida wa kwenda vituoni au wahuduma kufata wahusika.

“Tunatoa chanjo kupitia shuleni kwani watoto wa umri huo wako shule na binti akipata chanjo atapata kinga kubwa kwa dozi moja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Sheikh Mohammed Mawinda amesema jamii imekuwa na shida ya sintofahau kupokea jambo hilo na jukumu lao ni kuwaelimisha.

“Sisi tuko na jamii kila siku na tunakaa nao kwasababu tumepata elimu tutawaelewesha kuwa serikali ina nia nzuri ya kutuletea maendeleo hivyo wanafanya hivyo kuokoa vijana wetu ambao watakuja kuwa taifa la baadae.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live