Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanjo ya corona si lazima kwa watoto

C9d03de9c2876c55b5c24ac0d8ed2597.jpeg Chanjo ya Corona

Sat, 7 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WATAALAMU wa afya wamesema si lazima watoto chini ya umri wa miaka 16 kupata chanjo ya Uviko-19 kutokana na ugonjwa huo kuwashambuliza zaidi watu wenye umri mkubwa hasa kuanzi miaka 50.

Sababu nyingine zilizotolewa na wataalamu hao ni kwamba utafiti wa chanjo hizo ulifanyika zaidi kwa watu wazima kuliko watoto licha ya kutokuwa na madhara hata kwa watoto.

Wataalamu hao walibainisha hayo jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) Dar es Salaam wakati wakijibu maswali ya waadishi wa habari kuhusu matumizi ya chanjo ya Uviko-19 iliyoanza kutolewa hivi karibuni nchini.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Tulizo Shem, alisema chanjo hiyo ni salama kwa watoto.

“Madhara makubwa ya Covid 19, hivi sasa tupo hospitalini tunaona wagonjwa wengi ni miaka 50, lakini pia 30 hadi 40 tunawaona na huwa madhara yao hayalingani, wenye miaka 50 madhara yao ni makubwa zaidi.

“Lakini pia ukiangalia Utafiti wa chanjo kwa kiasi kikubwa ulifanyika kwa watu wazima lakini kama nchi kipaumbele ni kwa makundi matatu tukisema wachanje wote haitatosha na si kwamba si salama kwa watoto… Marekani wamechanja watoto kuanzia miaka 12 ni mahitaji yamefanya kuwa hivyo,” alibainisha Dk Shem.

Alisema chanjo hii hutolewa mara moja kutokana na namna ilivyotengenezwa na kufanyiwa majaribio na kwamba, mtu anapougua, inaweza kumkinga dhidi ya aina nyingine ya virusi kama vitajibadilisha, lakini si watu wote.

Mkurugenzi wa Kuratibu Mafunzo ya Utafiti katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa Binadamu (NIMR), Dk Paul Kazyoba alisema watu wenye maambukizi ya virusi vya corona au magonjwa mengine ya kuambukizwa, wasubiri wapone kwanza ili wachanje.

“Mwongozo wa chanjo unasisitiza kama mtu anadalili ambazo ni zile za Covid-19, anatakiwa aahirishe kuchanjwa na inashauriwa kama unaumwa magonjwa ya kuambukiza na dalili za ugonjwa zinajionesha, aahirishe kuchoma chanjo.”

“Sababu za kuahirisha mfano una malaria na huwa ina homa kali ukichanja kuna muda mwili lazima ushtuke, kwa sababu kuna kitu kinaingia mwilini kwenye hayo mapambano, kuna homa kidogo, misuli inauma sasa kama una ugonjwa mwingine inawezekana ikakuletea shida, kwa mtaalamu wa afya itakuwa vigumu kugundua kama inatokana na chanjo au ugonjwa uliokuwa nao,” alisema.

Kuhusu Chanjo kuathri mifumo ya uzazi ikiwemo nguvu za kiume na mzunguko wa hedhi DK Kazyoba alisema hakuna ushahidi kuhusu hilo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz