Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanjo ya Ini yathibitishwa kupunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa 90%

HPV Chanjo ya Ini yathibitishwa kupunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa 90%

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya utafiti wa Saratani ya nchini Uingereza imetoa tathimini mpya ya chanjo ya ini ya'human papillomavirus' maarufu kama HPV kuwa inauwezo wa kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 90.

Utafiti huo waliouita wa kihistoria unatajwa kuokoa maisha ya wagonjwa wengi wa saratani na inaelezwa kuwa chanjo hiyo inaweza kuondoa kabisa ugonjwa huo.

Aidha umeelekeza kuwa kwa wale waliopatiwa chanjo hiyo watahitajika kufanya vipimo vichache vya uchunguzi wa mlango wa kizazi.

Sanjari na hayo umebainisha kuwa wasichana wenye umri wa miaka 11 na 13 waishio nchini wamekuwa wakipatiwa chanjo hiyo huku kasi ya maambukizi ikupungua kwa asilimia 87.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live