Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanjo ya AstraZeneca kuanza kuuzwa kwa faida

Vaccine RONA Chanjo ya AstraZeneca kuanza kuuzwa kwa faida

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

AstraZeneca imeanza kuachana na mpango wa kutoa chanjo zake za Covid-19 kwa nchi kwa utaratibu usioipatia faida. Maana yake sasa itaanza kuuza chanjo hiyo kwa faida.

Kampuni hiyo kubwa ya dawa imesaini mikataba mingi ya kifaida kuanzia mwakani, na ikitarajiwa kupata kipato kutokana na chanjo hiyo, imesema kampuni hiyo.

Awali Kampuni hiyo ilisema, ingeanza kutengeneza pesa kutokana na chanjo itakapofikia wakati kwamba ugonjwa wa Covid-19 hautokuwa janga tena.

Mtendaji wake mkuu Pascal Soriot aliwahi kunukuliwa akisema: "tuliamua kusambaza chanjo hii bila faida kwa sababu kipaumbele chetu kikubwa ilikuwa ni kulinda afya ya umma."

Aliiambia BBC kwamba "hawajuti kabisa kutoa chanjo hizo bila kupata faida" huku washindani wake wengine wakitengeneza faida, licha ya kukabiliana na ukosoaji wa kisiasa kutoka kwa baadhi ya nchi.

Alisema chanjo hiyo ya AstraZeneca ambayo inatengenezwa kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, imeokoa maisha ya mamilioni ya watu duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live