Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA yathibitisha Mhe Mbowe kulazwa KCMC

4242 MBOWE TZW

Fri, 9 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi Kilimanjaro.



Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amethibitisha juu ya taarifa hiyo na kusema kuwa Mbowe amelazwa toka jana Machi 4, 2018 na mpaka sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

“Ni kweli Mbowe amelazwa toka jana yupo pale KCMC na anaendelea kupatiwa matibabu, siwezi kuzungumzia kinachomsumbua kwa kuwa ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari labda hivyo tutambue tu anaumwa amelazwa KCMC” alisema Mrema

Mbowe siku za karibuni alikuwa na mizunguko mingi mno kuanzia kwenye kampeni za uchaguzi wa Kinondoni na Siha lakini pia safari za Mbeya mara kadhaa kwenye kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini na Katibu wa CHADEMA Nyanda za Juu Kusini.

Chanzo: bongo5.com