Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CDC: Chanjo za Corona zizingatie muda wa matumizi

Nkengasong Nchi kadhaa zimekua zikiharibu chanjo ambazo muda wa matumizi umekaribia

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) Barani Afrika kimetaka Chanjo za COVID-19 zinazotolewa kuwa na muda wa matumizi kati ya miezi mitatu hadi sita ili Mataifa yaweze kupanga usambazaji kikamilifu na kuepuka dozi kuharibika.

Mkurugenzi wa CDC Afrika, John Nkengasong amesema Dozi Milioni 2.8 kati ya Milioni 572 zilizotolewa hadi sasa ziliisha muda wake Barani humo kutokana na kuwasili zikiwa zimesalia na muda mchache wa matumizi.

Kwa mujibu wa Kituo hicho asilimia 10.4 ya Waafrika wameshapata Chanjo dhidi ya Virusi vya Corona kikamilifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live