Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bugando wagundua mdudu anayegandisha damu watoto

Udu Pic Data (600 X 400) Bugando wagundua mdudu anayegandisha damu watoto

Thu, 18 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando (BMC) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi ya Afya (Cuhas) wamegundua mdudu mpya ambaye husababisha kuganda kwa damu kwa watoto wachanga.

Akitoa taarifa leo Novemba 18, 2021 wakati wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa BMC yaliyohudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mkuu wa BMC, Dk Fabian Massaga amesema, ugunduzi wa mdudu huyo ni matokeo ya tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika kubaini vyanzo vya magonjwa yasiyo ambukiza kama vile saratani, shinukizo la damu na kisukari.

“Ni matumaini yetu kwamba miaka 50 ijayo hospitali ya bugando itakuwa na hadhi ya kimataifa yenye uwezo mkubwa zaidi wa kuhudumia watanzania pamoja na nchi jirani katika zana nzima ya medical tourism,’

Dk Massaga amesema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kuelekea maadhimisho hayo, madaktari bingwa walipita katika hospitali za mikoa ya Kanda ya Ziwa na kutoa huduma za matibabu bure ambapo zaidi ya 35,000 walipatiwa huduma mbalimbali huku wananchi 83 walipatiwa huduma za upasuaji.

Amesema hospitali hiyo inavitanda 950 na wafanyakazi 1,800 kati ya wafanyakazi 2554 wanaohitajika huku wafanyakazi 1,191 waliopo wanalipwa mshahara na Serikali na waliobaki wanalipwa mshahara na taasisi.

“Hospitali hii inahudumia zaidi ya wananchi milioni 18 katika mikoa nane ya Kanda ya Ziwa lakini pia tunahudumia wananchi kutoka nchi za jirani kama vile Uganda, Kenya, Burundi na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,”amesema

Ameishukuru Serikali kuendelea kufanikisha huduma za saratani ambapo awamu ya kwanza ilitoa Sh5.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba sita vya matibabu ya saratani na ofisi huku awamu ya pili ikitoa Sh1 bilioni katika ujenzi wa wodi unaoendelea.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya BMC ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Renatus Nkwande amesema hospitali hiyo inauhitaji wa miundombinu ya kutolea huduma kwa wagonjwa kutokana na idadi ya wagonjwa kuongezeka.

Amesema hospitali hiyo imeanzisha miradi miwili ya ujenzi, ujenzi wa Taasisi ya moyo itayogharimu Sh10.5 bilioni na ujenzi wa jengo la mama na mtoto litakalogharimu Sh6.5 bilioni.

Ameiomba Serikali kufikiria ushuru wa shirika kwa taasisi zinazotoa huduma mahususi kama afya zifikiriwe kwakuwa huduma hizo zinahitaji kuboreshwa siku hadi Siku.

"Hili jambo lifikiriwe upya huduma hizi zinahitajika kuboreshwa siku hadi siku, baadhi ya tozo zinaweza zisifanikishe huduma kwa wananchi. unakusanya fedha lakini bado zinatozwa wakati uhitaji wa kufanya maboresho kwenye taasisi bado ni mkubwa,"amesema

Chanzo: mwananchidigital