Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bima ya Afya kwa wote kutibu magonjwa yote

Tushirikiane Huduma Bure Kwa Watoto Chini Ya Miaka Mitano Mollel.jpeg Bima ya Afya kwa wote kutibu magonjwa yote

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema kuwa Bima ya Afya kwa Wote ndio suluhu ya changamoto za magonjwa yote, kwani wananchi watatibiwa magonjwa yote ikiwemo ugonjwa wa Selimundu bila gharama kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya taifa.

Dkt. Mollel amesema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Sikonge, Mhe.Joseph George Kakunda katika mkutano wa 10, kikao cha 9, Bungeni Jijini Dodoma.

Amesema, licha ya Wizara ya Afya kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga katika mfuko wa bima ya afya, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Serikali yake ya awamu ya sita ameendelea kutoa fedha kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya matibabu ya magonjwa hayo.

Ameendelea kusema kuwa, tayari Bilion 11.5 zimetolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia kupitia Serikali yake kwaajili ya ununuzi wa kifaa chenye uwezo wa kupima vinasaba ili kutambua tatizo hilo na kulitibu.

Aidha, Dkt. Mollel amesema, tayari Hospitali za Rufaa za Mikoa zimeanza kutenga 10% ya mapato yake ya bima kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa wa seli mundu ili waweze kupata matibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live