Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bima ya Afya kwa watoto wasiojiweza yatolewa mkoani Morogoro

Ulanga Bima Mbunge wa Ulanga akigawa kadi za bima ya afya kwa watoto wenye uhitaji

Sun, 6 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Salim Alaudin Hasham amewakatia bima za Afya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 74 wanaolelewa katika kituo cha Ukwama wilayani humo.

Akizungumza baada ya kugawa bima hizo Salim Alaudin ambaye pia ndie mlezi wa kituo hicho amesema lengo kubwa la kufanya zoezi hilo ni kuwahakikishia uhakika wa kupata matibabu kwa haraka bila Changamoto zozote ili kuwapunguzia mzigo Mkubwa wasimamizi wa kituo hicho.

Mbali na kuwakatia bima za Afya pia Salim Alaudin amefanya marekebisho ya Jengo wanaloishi watoto hao na kuwajengea vyoo bora ili mazingira yawe salama zaidi nanyakuvutia na watoto hao wasijisikie upweke kwa kipindi chote watakachoishi hapo.

Aidha Mhe Salim Alaudin ameongeza kuwa ukarabati wote huo utagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 15.5 na fedha zote hizo zinatoka mfukoni mwake pia ataendelea kukisimamia kituo hicho ili kuhakikisha usalama na mazingira bora yanapatikana kwa watoto hao.

Kwa upande wake Msimamizi wa kituo hicho Bi. Redepta Choma amemshukuru Mbunge Salim Alaudin kwa moyo wake wa kujitoa kukisaidia kituo kwani ni watu wachache wanaoweza kufanya hivyo na amemuomba asichoke kuwasaidia na Mungu atambariki.

Redepta pia ameongeza kuwa zipo changamoto nyingi zilizokuwa zinawakabili awali ikiwemo huduma za Afya lakini kwasasa mlezi wao amejitahidi kuzipunguza kwa kiasi kikubwa.

Mama mlezi wa kituo hicho Bibi Elizabeth Choma amesema anamshukuru Mungu kwa kumleta Baba mlezi wao kwani walikuwa na hali mbaya lakini kwasasa Baba mlezi anawapambania na wanaona baadhi ya Changamoto Sinai soka taratibu.

Kituo hicho cha kulea watoto yatima na wenye mahitaji maalum UKWAMA kilianzishwa mwaka 1976 na kanisa katoliki kwa lengo la kuwasaidia wahitaji hususani watoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live