Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bil 4.6/- zatumika kukata CHF kwa watoto 361,539

703cac3f24bac417dc8daff41aa962c9 Bil 4.6/- zatumika kukata CHF kwa watoto 361,539

Sat, 13 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JUMLA ya Sh bilioni 4.6 zimetumika kugharamia kadi za bima ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF imeboreshwa) kwa watoto 361,539 wanaoishi katika mazingira hatarishi mikoa 24 nchini.

Hayo yameelezwa jijini hapa na Naibu Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk Festo Lugange wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa kadi hizo.

Alisema hatua hiyo ni katika kuhakikisha watoto wanaoishi katika maaingira magumu wanafikiwa na huduma za afya.

“Huu ni mchango kubwa, idadi ya kaya na wanufaika ni kubwa na haya ni mapinduzi makubwa sana ya wadau kushirikiana na Serikali. Mpaka sasa kiasi cha fedha Sh bilioni 4.6 tayari zimeshatumwa kwenye akaunti za CHF iliyoboreshwa kwa ajili ya mikoa 24 nchini,” alisema.

Aidha, Dk Lugange akitumia fursa hiyo kulishukuru Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID) na Pact Tanzania kwa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha watoto wanaoishi katika maingira magumu wanafikia hudumavza afya.

Alisema mbali ya fedha hizo kwenda kunufaisha watoto walio katika mazingira hatarishi na kaya zao, fedha hizo zitaweka uhakika wa upatikanaji wa huduma za afya katika kuwezesha upatikanaji wa dawa, vitenganishi na vifaa tiba kwa ubora zaidi.

"Natoa wito kwa watoa huduma wote nchini kusimamia na kuhakikisha watoto wote hawa waliokatika mazingira hatarishi na wananchi wote walio katika mfumo wa walioko katika mfumo huu wa bima iliyoboreshwa wanapata huduma bora za afya bila shida yoyote,"alisema.

Aliwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia mfuko na kuhamasisha Watanzania wote kujiunga na mfuko wa CHF iliyoboreshwa.

Awali Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk Ntuli Kapologwe alisema wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wamechangia Sh bilioni 11 kwa kujiunga na huduma za mfuko huo wa CHF.

“Kabla ya CHF iliyoboreshwa michango ya wananchi ilikuwa haizidi shilingi bilioni 3 lakini baada ya kuanzisha CHF iliyoboreshwa na kuboresha mafao yatolewayo michango imefikia Sh bilioni 16 kwa mwaka ikiwa ni michango ya wananchi, wadau na serikali,” alisema.

Dk Kapologwe alisema kuongezeka kwa michango hiyo ni dalili kuwa suala la upatikanaji wa dawa na huduma za afya zitaimarika.

Chanzo: habarileo.co.tz