Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Exim yajiunga rasmi kuchangia damu Tanzania

61176 Exim+pic

Tue, 4 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kilimanjaro.  Benki ya Exim Tanzania pamoja na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) wameingia kwenye makubaliano rasmi ya utekelezaji wa pamoja wa mpango wa uchangiaji wa damu utakaohusisha matawi yote ya benki hiyo Tanzania.

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo ya uwajibikaji kwa jamii unaofahamika kama ‘Exim Cares’

Ushirikiano huo umezinduliwa rasmi leo Jumatatu Juni 3, 2019 katika tukio la uchangiaji wa damu lililoandaliwa na benki hiyo kwenye tawi lake lililopo barabara ya Old Moshi katika Manispaa ya Moshi, mkoa wa Kilimanjaro.

Hatua hiyo ni urasimishaji wa jitihada za benki hiyo kwa kipindi cha miaka nane mfululizo katika uchangiaji wa damu hapa nchini.

Akizungumzia mpango huo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Staniley Kafu amesema mpango huo unakwenda sambamba na kauli mbiu ya benki hiyo inayosema Exim kazini leo kwa ajili ya kesho” ambao pamoja na mambo mengine unalenga kuchangisha damu na kutoa elimu ya umuhimu wa kuchangia damu katika mpango wa taifa.

“Kampeni hii ni sehemu ya uthibitisho kuwa benki ya Exim iko makini kutafuta njia za ubunifu za kuhudumia wateja wake,  muhimu zaidi, inajitolea kuhakikisha inashiriki kuleta mabadiliko chanya katika jamii,’’  amesema Kafu.

Pia Soma

Kafu amesema benki hiyo itawezesha mpango na utekelezaji wa uchangiaji damu kwenye kambi nane za uchangiaji damu katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Tanga, Mtwara na Zanzibar huku ofisi ya Mpango wa Taifa Damu Salama  wakisimamia masuala yote ya kitabibu katika mpango huo.

“Zaidi benki ya Exim kwa kushirikiana wadau wote wa mpango huu wakiwemo Mpango wa Taifa Damu Salama, Wizara ya Afya na wadau wa habari tutahusika na kuratibu mikakati ya uelimishaji na uhamasishaji wa wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi katika suala hili muhimu kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya kuchangia damu duniani.’’ Alisema Kafu

Kwa upande wa Menaja wa NBTS Kanda ya Kaskazini, Dk  Edson Mollel amesema ofisi hiyo inahitaji kukusanya chupa (units) 526,000 za damu ili kukidhi mahitaji ya kila mwaka kwa nchi nzima ambapo kiasi kilichopatikana mwaka jana ilikuwa ni chupa 307,835 sawa na asilimia 58 ya mahitaji.

“Mwaka huu lengo ni kukusanya chupa 357,000 za damu na kupitia maadhimisho ya mwaka huu pekee tumejipanga kukusanya chupa 41,920 ndiyo maana tunaridhishwa sana wanapojitokeza wadau kama benki ya Exim ili kutuunga mkono, uhitaji wa damu bado ni mkubwa.

“Hatua hii ni mfano wa kuigwa kwa kuwa benki ya Exim na wafanyakazi wake wanakuwa sehemu ya jamii wanayoihudumia kwa ukaribu zaidi na  pia wanathibitisha rasmi mioyo yao ya  kujitolea kwa hali na mali kwa jamii wanayoihudumia,’’ amesema Mollel.

Chanzo: mwananchi.co.tz