Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraza la uuguzi lawapa onyo wakunga sita

10377 Wakunga+pic TanzaniaWeb

Sun, 1 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limewakuta na hatia na kuwapa karipio kali la maandishi wauguzi wakunga sita wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

 

Watumishi hao wamepewa karipio hilo kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ya kitaaluma wakati wakitoa huduma kwa mgonjwa katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika jana Juni 28, 2018 Kibaha mkoani Pwani.

 

Mwenyekiti wa baraza hilo, Abner Mathube amesema walisikiliza shauri la ukwiukwaji wa maadili ya kazi kwa mama mjamzito aliyelalamika kutokupatiwa huduma stahiki alipofika hospitali hali iliyochangia mtoto wake kufariki dunia.

 

Pamoja na karipio hilo, wameonywa endapo watarudia kosa hilo, baraza hilo halitasita kuwachukulia hatua kali zaidi, ikiwemo kuwafutia usajili.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz