Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bangi kusababisha kukosa watoto

34224 Pic+bangi Tanzania Web Photo

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

New York, Marekani. Matumizi ya bangi kwa wanaume waliopo kwenye umri wa kupata watoto, yanaweza kuathiri mbegu zao na kusababisha kukosa uwezo wa kupata watoto, utafiti mpya umeonyesha.

Utafiti huo uliofanywa katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Duke huko Marekani, umeonyesha kuwa matumizi ya bangi kwa wanaume, yanawaweka kwenye hatari ya kupata watoto baadaye, kutokana na nguvu kubwa ya mmea huo katika kubadili mbegu za wanaume.

“Tulichokigundua ni kwamba, madhara ya matumizi ya bangi kwa wanaume si ya ujumla lakini kuna kitu katika matumizi yake ambacho kina madhara kwenye mbegu za kiume,” amesema Dokta Scott Kollins, profesa wa sayansi ya akili na tabia Chuo Kikuu cha Duke.

Utafiti huo uliotolewa Desemba 19 ulihusisha mbegu za wanadamu na zile za panya, ulijikita katika kujua madhara ya mmea wa bangi kwa wanadamu wa jinsi ya kiume na kwa panya wa jinsi hiyo hiyo ya kiume, uligundua kwamba kemikali zake zinaathiri na kubadili vinasaba vya mbegu za kiume kwa mtumiaji.

Mabadiliko ya vinasaba katika mbegu za kiume huwa ni ya kiasili na husababishwa na baadhi ya mambo ikiwemo umri, mazingira au aina ya maisha mtu anayoishi, hivyo, matumizi ya bangi na magonjwa aina ya kansa pia husababisha mabadiliko hayo.

“Hatujui hii inamaanisha nini, lakini ukweli kwamba vijana wengi wa umri wa kupata watoto wapo katika nafasi ya kupata bangi kihalali hapa Marekani, hili ni jambo la kutazamwa kwa umakini mkubwa,” Dokta Kollins amesema.

Tafiti zilizofanyika maabara zikihusisha panya na wanaume 24 zinaonyesha kuwa, matumizi ya bangi yanaathiri vinasaba katika mbegu za kiume na kusababisha mabadiliko kitu ambacho kinaweza kusababisha matatizo kwenye uzazi.



Chanzo: mwananchi.co.tz