Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bangi inasababisha mshituko wa moyo

Shamba La Bangi Bangi inasababisha mshituko wa moyo

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utafiti mpya uliofanyika Marekani umegundua kuwa kuvuta au kula bidhaa zozote zenye bangi kunaweza kusababisha athari kubwa kwenye moyo wa Binadamu kama vile kupata mshtuko wa moyo na stroke ( yani ugonjwa wa kiharusi) ambapo yote haya yanaweza kutokea hata kwa Mtu ambae hajawahi kuwa na magonjwa ya moyo au hata kama hajawahi kuvuta sigara.

Utafiti huo pia umegundua kuwa hatari ya kupata ugonjwa wa kiharusi kwa wanaotumia bangi kila siku za maisha yao uliongezeka kwa 42% huku hatari ya mtu kupata mshtuko wa moyo kwa kuvuta kila siku ikiongezeka kwa 25%.

Robert Page II, Profesa wa Chuo Kikuu cha Colorado Skaggs School of Pharmacy na Sayansi ya Madawa huko Aurora, amesema ongezeko la matumizi ya bangi limehusishwa na mshtuko wa moyo pamoja na ugonjwa wa kiharusi ambapo Vijana wa makamo walio chini ya miaka 55 na Wanawake chini ya miaka 65 ambao walitumia bangi, walikuwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo, mshtuko wa moyo na stroke kwa asilimia 36% na hiyo ni bila kujali kama waliwahi kutumia bidhaa za kitamaduni za tumbaku kama vile sigara.

Taasisi ya magonjwa ya Moyo nchini Marekani inawashauri Watu kujiepusha na uvutaji wa sigara na bangi au kula vyakula vilivyowekewa bangi ikiwa ni pamoja na bidhaa za bangi kwa sababu ya madhara yanayoweza kutokea kwenye moyo, mapafu na mishipa ya damu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live