Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balozi ataka watanzania kuzingatia tahadhari corona

8af9de2874743acb0751a2e448641c36 Balozi ataka watanzania kuzingatia tahadhari corona

Mon, 22 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BALOZI wa Tanzania nchini Zimbabwe, Profesa Emmanuel Mbenah amewataka watanzania kuchukua tahadhari na kuzingatia miongozo ya afya na kumtanguliza Mungu katika kukabili magonjwa yaliyoikumba dunia ukiwamo ugonjwa wa corona .

Alisemani vyema kumtegemea Mungu zaidi kwa kuwa yeye ndiye jawabu la uponyaji wa maambukizi hayo.

Profesa Mbenah ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika ibada ya kwaresima iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika Jijini Dodoma juzi.

Alisema magonjwa ya maambukizi ikiwemo Corona ni janga ambalo limeikumba karibu dunia yote,hivyo kunahitajika kuwa na umakini katika utumiaji wa madawa ya kujifukiza au kunywa huku tukimtanguliza Mungu mbele.

Balozi huyo ambaye pia ni mchungaji wa kanisa la Angalikana akizungumzia kipindi cha mfungo mtukufu wa Kwaresma alisema kuwa ni kipindi cha kufanya toba ya kweli na kujitenga na dhambi.

Pia mbali na kufanya toba ya kweli alisema kuwa mfungo wa Kwaresma isiwe sehemu ya tukio tu bali wakristo wote wanatakiwa kuhakikisha muda wote wanakuwa karibu na Mungu kwa kuomba,kutubu na kuwasamehe wale waliowakosea.

Naye mama Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika Pendo Chilongani amesema kuwa ni vyema watanzania wakaendelea na utamaduni wa kuchukua hatua ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Chanzo: habarileo.co.tz