Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bajeti ya maendeleo Wizara ya Ardhi yafyekwa

Fri, 31 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imesema hairidhishwi na Serikali kupunguza bajeti ya maendeleo katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Sh 6.2bilioni.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 31,  2019, wakati Mjumbe wa kamati hiyo, Shabani Shekilindi akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwa makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2019/2020.

“Bajeti  ya maendeleo imeshuka kutoka Sh30.5bilioni kwa mwaka wa fedha 2018/19 hadi Sh24.3bilioni kwa mwaka 2019/2020,” amesema.

Amesema huo sio mwenendo mzuri kama Serikali imedhamiria kuleta mageuzi katika sekta ya ardhi hususani katika kupima na kupanga matumizi ya ardhi.

“Ni matarajio ya Kamati  Serikali itaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ,”amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz