Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Audio: Mtangazaji ajifungua ‘live’ akitangaza redioni

3671 28151568 2120513418178208 8759105438164713472 N TZW

Mon, 26 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Duniani kuna mengi yanatokea na kushangaza, huku mengine yakikuacha mdoma wazi. Mtangazaji wa kipindi cha Alfajiri katika kituo cha radio cha The Arch kilichopo katika mji wa St Louis nchini Marekani, Cassiday Proctor amejifungua mtoto wiki hii kwenye kipindi chake.



Mtangazaji huyo alipata bahati hiyo baada ya kituo chake cha habari kiliposhirikiana na hospitali ambayo alijifungua ili matangazo yake yaweze kuruka moja kwa moja hewani wakati akijifungu.

Baada ya kujifungua huku akisikika moja kwa moja radion, Cassiday amesema yeye huwaambia kila kitu wasikilizaji kuhusu maisha yake.



Mtoto huyo ambaye amepewa jina la Jameson, amezaliwa akiwa na uzito wa kilogram 3.345. Hapa chini ni sauti ya mtangazaji Cassiday wakati akijifungua akiwa hewani.

Chanzo: bongo5.com