Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atolewa uvimbe kwenye ubongo kwa kupitia pua Mloganzila

MLOGA Ubongo Atolewa uvimbe kwenye ubongo kwa kupitia pua Mloganzila

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kwa kutumia matundu ya pua ameruhusiwa mwishoni mwa wiki baada ya afya yake kuimarika ambapo amekaa hospitalini takribaini wiki moja baada ya upasuaji huo.

Akizungumza kwa niaba ya familia Sifa Majura ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kuokoa maisha ya mume wake ambaye amehangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio.

Sifa, ameongeza kuwa matibabu aliyopata mumewe ni ya kiwango cha juu ambayo hapo awali matibabu haya yalikuwa yanafanyika nje ya nchi lakini kwa sasa matibabu ya aina hii yanapatikana hapa Mloganzila na mtu kupona kabisa.

Amebainisha kuwa ameamini kuwa mgonjwa anayeletwa Mloganzila ni yule aliyeshindikana kutoka maeneo mengine ya kutolea huduma, hiyo ni kutokana na kuwa na wataalamu waliobobea wenye sifa na weledi wa kutoa huduma za afya.

“Naishukuru na kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wetu mpendwa Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji huu mkubwa aliofanya wa kuwajengea uwezo wataalam wetu wa ndani na kununua vifaa tiba uliowezesha huduma hizi kufanyika kikamilifu na kwa mafanikio makubwa” amesema Sifa.

Ameongeza kuwa mume wake alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kwa kutumia matundu ya pua baada ya kupata ajali alipokuwa akielekea mkoani Kilimanjaro ambapo walimpeleka hospitali mbambali bila mafanikio na hatimaye alipofika Mloganzila tatizo lilibainika na kupatiwa matibabu stahiki.

Amefafanua kuwa kwa sasa afya ya mgonjwa wake imeimarika sana kwa kuwa anaongea ambapo hapo awali alikuwa haongei kabisa, aidha ameeleza kuwa atakuwa anarudi kliniki kwa ajili ya ushauri na kufuatiliaji wa maendeleo yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live