Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atakayetiririsha maji machafu mtaani faini Sh 200,000

60342 Pic+ummy

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtu mmoja amefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu jijini Dar es Salaam, huku 32 wakilazwa katika kambi maalum za kipindupindu jijini humo.

Hayo yamesemwa leo Mei 29 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake anayoendelea nayo jijini Dar es Salaam kuangalia hali ya ugonjwa wa kipindupindu na homa ya dengue.

"Tumepokea wagonjwa 32 katika mkoa wa Dar es Salaam, kambi ya Amana wapo 13, Temeke 18 na Mwananyamala mmoja, hii ni kutokana na kutozingatia usafi," amesema.

Kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo, waziri huyo ametoa maagizo akizitaka halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam kuweka sheria kali kwa wanaotiririsha maji machafu wakati wa mvua.

"Mstahiki Meya kasema adhabu niĀ  Sh30,000 nimewataka waongeze adhabu iwe Sh200,000 tunataka mtu aone ni bora kuita gari la maji taka Sh150,000 kuliko kulipa hiyo faini, nimeshatoa maagizo yeyote atakayetiririsha maji machafu achukuliwe hatua kali," Amesema Ummy.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Yudas Ndungile amesema sehemu kubwa ya wagonjwa wa kipindupindu waliopatikana wanatoka katika eneo la Mchikichini na mabondeni ambako magari ya kusomba taka hayapo, hivyo mipango inafanywa kuangalia namna ya kuyafikia maeneo hayo.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz