Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Asimilia 90 wanakufa kwa malaria Afrika"- Bangali

WhatsApp Image 2021 07 12 At 12.43.39.jpeg "Asimilia 90 wanakufa kwa malaria Afrika"- Bangali

Mon, 12 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

 

Akizungumza leo mkoani Morogoro na madaktari hao Mkurugenzi wa shirika hilo upande wa Tanzania, Kumar Bangali, amesema hatua hiyo imekuja baada ya tafiti zilizofanyika kuonesha bara la Afrika ndio linaongoza kwa vifo vitokanavyo na malaria kwa zaidi ya asilimia 90.

Amesema miongoni wa sababu zinazopelekea ugonjwa huo kuendelea kuchukua maisha ya watu wengi ni matumizi yasiyosahihi ya dozi na kushindwa kumaliza dozi kama inavyoshauliwa na wataalamu kwa kisingizio ya wingi wa dawa ambazo uchukua muda refu kuisha.

“Takwimu zinaonesha Afrika ndio bara linaloongoza kwa vifo kwa asilimia 90 ndio maana shirika letu limejikita katika kutafuta suruhu ya changamoto hii kwa kuwashirikisha madaktari bingwa na kuwapa elimu kwa kusisitiza matumizi sahihi ya dozi ambayo haitamchosha mgonjwa” amesema Bangali

Abby Kosana, ambaye ni mtaalam wa dawa katika shirika hilo, amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto ya kutomaliza dozi kwa baadhi ya wagonjwa tayari wataalam wamefanikiwa kutengeneza dozi fupi ambayo haitamchosha mgonjwa.

Amesema dawa ambazo zipo katika dozi mpya zina vidonge sita ambapo mgonja akitumia zitasaidia kumalizi kabisa ugonjwa tofauti na awali ambapo wagonjwa walikuwa wakikatisha dozi wakidhani tayari wamepona.

“Kama tafiti zilivyoonesha watu wengi walikuwa wanakimbia kumaliza dozi kwa sababu ya vidonge kuwa vingi na vinawachosha ndio maana tukaja na dawa mbalimbali kama hii ya Artefan ambayo inavidonge sita tu, hii itasaida sana watu kumaliza dozi ili maralia isiweze kujirudia” amesema Kosana

Chanzo: ippmedia.com