Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 99 wanavuta hewa chafu duniani- WHO

Bfbd6b6adb24027e1f101696ce8afd32 Asilimia 99 wanavuta hewa chafu duniani

Tue, 5 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani (WHO), limeonya kwamba karibu kila mtu duniani anavuta hewa ambayo haikidhi viwango vya ubora na kutoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa kupunguza matumizi ya mafuta, yanayosababisha uchafuzi, matatizo ya kupumua na kuathiri mtiririko wa damu kwa mamilioni ya watu.

WHO imesema vifo vinaweza kuzuilika kila mwaka, ikiwa hatua stahiki zitachukuliwa.

Kutokana na tathimini ya ubora wa hali ya hewa katika miji, majiji na vijiji kote ulimwenguni, ambayo imehusisha jumla ya maeneo 6,000, imeonesha kuwa asilimia 99 ya watu duniani wanavuta hewa isiyo na ubora na mara nyingi ina chembechembe zinazoweza kuingia ndani kabisa ya mapafu, kwenye mishipa na kusababisha magonjwa, NBC News iliripoti Jumanne.

“Ubora wa hewa ni duni zaidi katika maeneo ya Mediterranean ya Mashariki na Kusini-Mashariki mwa Asia, ikifuatiwa na Afrika,”taarifa ya WHO iliongeza.

"Baada ya kunusurika na janga (la Covid-19), ni jambo lisilokubalika kuwa bado kuna vifo vinavyoweza kuzuilika vikichangiwa na uchafuzi wa hewa," alisema Dk. Maria Neira, Mkuu wa Idara ya Mazingira WHO.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live