Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 95 ya walioumwa Corona hawakuchanjwa

CORONA CHANJO?fit=660%2C371&ssl=1 Asilimia 95 ya walioumwa Corona hawakuchanjwa

Wed, 26 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema watu 3147 walilazwa hospitalini kutokana na Uviko-19 kati ya Septemba 2021 mpaka Januari 23, 2022 ambapo kati yao 2990 sawa na asilimia 95 walikuwa hawajachanja.

Pia, imesema kuwa mpaka sasa ni watu 1,922,019 waliochanja sawa na asilimia 3.3 ya Watanzania waliolengwa.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Januari 26, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu baada ya kupokea shehena ya chanjo 800,000 za Sinopharm ambazo ni sawa na dozi 400,000 kutoka Serikali ya watu wa China.

“Wagonjwa waliokuwa mahututi katika vyumba vya uangalizi maalumu kwa siku ya Januari 23 mwaka huu ICU walikuwa 31 kati yao 30 walikuwa hawajachanjwa.

Vifo vilivyotokea vilikua 76 kati ya hivyo vifo 73 viliwahusisha wagonjwa ambao hawakuchanja,” amesema Waziri Ummy.

Amewataka Watanzania kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya kupima kwa kuwa si kila homa au mafua ni Uviko-19.

“Una homa kapime watu sasa hivi wanakunywa Azuma na dawa zingine za antibaotiki, si kila homa ni corona tuache kujitibu kapime upate matibabu sahihi, tunatengeneza usugu wa dawa baadaye tutakua tunatibu watu hawaponi,” amesema.

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dk Beatrice Mutayoba amesema chanjo hizo zina uwezo wa kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.

“JJ inakaa miezi mitano tunafanya utaratibu wa kuzigawa ndani ya muda mfupi tunakuwa tumezimaliza, chanjo za Sinopharm ni miaka miwili na Pfizer zinakaa miezi 8,” amesema Dk Mutayoba.

Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian amesema mpaka sasa zaidi ya asilimia 80 ya watu wa China wamechanja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live