Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 50 waliopata TB ni watoto

Tb Pc Data.png Asilimia 50 waliopata TB ni watoto

Sun, 27 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watoto 1,900 waliogundulika kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) katika kipindi cha mwaka jana (2021) katika mkoa wa Tabora, ambao ni sawa na asilimia 50 ya walioambukizwa ugonjwa huo.

Akizungumza leo Februari 27 katika uzinduzi wa mradi wa USAID C3HP mjini hapa, Mganga Mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Honoratha Rutatinisibwa amesema kwa mwaka jana watu wapatao 3,754 waligundulika na ugonjwa huo huku watoto waligundulika wakiwa ni asilimia 51 sawa na watoto 1,914.

hayo kwa mkoa wa Tabora ambao utatetekelezwa na asasi ya Egpaf kwa kipindi Cha miaka mitano ijayo.

Kati ya idadi hiyo ya walioambukizwa, amesema asilimia 31 walikuwa ni watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).

Amesema kwa mwaka huu wamewekewa lengo la kuwafikia wagonjwa 4,228 kwa mkoa mzima na kuwa watajitahidi kufikia lengo hilo.

"Mradi huu utakuwa na manufaa makubwa kwetu na tutatumia kuhakikisha wagonjwa zaidi wa Kifua Kikuu wanafikiwa na kupatiwa matibabu," amesema.

Advertisement Naye Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la EGPAF Tanzania linalotekeleza mradi huo, Dk Sajida Kimambo, amesema mradi huo ni mafanikio ya mradi wa USAID Boresha Afya ambao umetekelezwa kwa miaka mitano na kumalizika Septemba 2021 katika mikoa sita, Tabora ukiwemo.

Ametaja mafanikio yaliyosababisha kuanza mradi huo mpya kuwa ni kufikia wagonjwa wapya wa Kifua Kikuu 93,000 huku mkoa wa Tabora ukifikiwa wagonjwa hao 13,873 katika miaka hiyo mitano.

Awali akizindua rasmi mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian ametaka kufuatiliwa kwa kaya zote zilizoathirika na ugonjwa huo ili kuona kama bado Kuna tatizo la ugonjwa huo.

Katika hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa Wilaya ya Tabora, Dk Yahaya Nawanda, Dk Burian amewataka wahudumu katika sekta ya Afya kuwa na huduma nzuri pamoja na lugha nzuri ili wagonjwa wavutiwe kwenda kupata matibabu.

Mradi huo utachukua miaka mitano na lengo lake baadhi ni kupunguza maambukizi mapya ya VVU sanjali na kuboresha huduma za Afya katika sehemu za kutolea huduma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live