Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 30 ya watoto chini ya miaka mitano mkoani Kigoma wana utapiamlo

73738 Utapiamlo+pic

Mon, 2 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Imeelezwa kuwa takribani asilimia 30 ya watoto chini ya umri wa miaka mitano katika Mkoa wa Kigoma wanasumbuliwa na utapiamlo wa lishe.

Tatizo hilo limeelezwa kuhusisha pia watoto wenye udumavu uliopitiliza, ambapo kwa hospitali ya Maweni pekee, kati ya watoto 120 wanaolazwa asilimia tano wana tatizo hilo.

Akizungumza na Mwananchi daktari wa watoto katika Hospitali ya Mkoa wa Kigoma ya Maweni, Erasto Umoja amesema utapiamlo ulikuwa mkubwa kipindi cha nyuma japokuwa kwa sasa  upo kwa asilimia 30.

"Kigoma chakula kipo ila nini wanakula watoto ndio tatizo, katika mwezi mmoja huwa tunapokea kati ya watoto watatu mpaka wanne wenye tatizo la udumavu uliopitiliza na hii ni hatari," amesema.

Akizungumzia namna walivyoweza kudhibiti tatizo hilo, Dk Umoja amesema watoa huduma za afya walipokea mafunzo kupitia mradi wa USAID Boresha Afya, waliweza kubaini mbinu mbalimbali za kupambana na tatizo hilo.

"Licha ya watoa huduma za afya kuwezeshwa pia tulipokea vitendea kazi, vifaa, maziwa na katanga maalum ambazo ni dozi maalum kwa watoto tunaowapokea ili kuokoa maisha yao, zamani tuliwatibu kama watoto wengine na hata kuwachanganya wodi moja hii ilisababisha wengi wao kupoteza maisha," amesema.

Pia Soma

Advertisement   ?
Pamoja na hayo amesema wameweza kutoa elimu kwa jamii, familia kujikinga na maradhi hasa kwa kinamama wanaonyonyesha na wenye watoto wadogo.

"Tunawahimiza kinamama wanyonyeshe mpaka kipindi cha miezi 6 bila kumpa chochote mtoto na kuendelea mpaka miaka miwili. Tunawahimiza kuwapa chakula mara kwa mara mtoto si chini ya mara nane hadi tisa kabla ya kuacha kunyonya,” amesema.

Kaimu mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kiza Kisesa amesema mradi wa USAID Boresha Afya umetoa mafunzo kwa watoa huduma katika Halmashauri nane za Mkoa huo.

Mfamasia huyo wa Mkoa amesema mradi huo umetoa mafunzo kwa watoa huduma ngazi ya jamii ambao kwa kiasi kikubwa wamefanikisha kupunguza tatizo lililokuwepo awali.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz