Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 26 ya watoto wana udumavu

F822e18ecba109a6ad018f83e39964d0 Asilimia 26 ya watoto wana udumavu

Mon, 8 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WATOTO wenye umri wa miaka mitano wanaofi kia asilimia 26.4 kati ya 400,000 katika Mkoa wa Morogoro, wanakabiriwa na udumavu na wenye ukondefu ni asilimia 3.7.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kusirye Ukio alisema hayo kwenye taarifa yake katika kikao cha wadau wa lishe cha mkoa huo, kilichofanyika juzi.

Wadau hao walikutana kujadili hali halisi ya lishe katika mkoa huo kupitia uwezeshaji wa Mradi wa Lishe Endelevu, unaofadhiliwa na Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani (USAID).

Alisema asilimia nyingine 12.1 ni watoto wenye uzito pungufu wakati wenye upungufu wa damu ni asilimia 65.7. Dk Ukio alisema upande wa uzito uliozidi kiwango ni asilimia mbili ya idadi yote ya watu waliopo mkoani humo ambao wanakadiriwa kuwa milioni 2.7.

Kuhusu unyoyeshaji watoto kimkoa, alisema akina mama wenye uwezo wa kunyonyesha watoto kwa muda wa miezi sita ni asilimia 55 na asilimia iliyobaki watoto wanaanzishiwa vyakula kabla hata hawajafikia miezi sita.

Alisema wanawake waliopo katika umri wa kuzaa, kwa maana ya miaka 15-49 , wenye upungufu wa damu wanafikia asilimia 30.

Dk Ukio alisema katika vifo vyote vilivyotolea mwaka jana, asilimia 55 vimetokana na kutokwa na damu nyingi na hiyo imechangiwa na wanawake kushika mimba wakiwa na hali duni ya lishe na kuwa na upungufu wa damu.

Alisema kwenye maeneo yenye changamoto ni vyema kuwapa dawa za vidonge vya kuongeza damu na kuhamasisha ulaji wa matunda dawa, ambayo gharama zake ni ndogo.

Dk Ukio alisema lengo ni kuwafanya wanawake wenye umri wa kuzaa wawe na damu ya kutosha muda wote ili kuwaokoa wanapokuwa na ujauzito na kutoa elimu ya lishe kwa jamii.

Akifungua kikao hicho, Katibu Tawala wa Mkoa, Emmanuel Kalobelo aliziagiza halmashauri zote za mkoa huo, kuandaa mpango wa kutekeleza afua za lishe na kutekelezwa ipasavyo.

Pia alihimiza ulaji wa vyakula wenye vitamini na madini na watoto wadogo na wachanga kupatiwa matibabu sahihi na taasisi na wadau kutoa elimu ya lishe na kuchangia masuala la lishe kwa vitendo.

Meneja wa Mpango wa USAID Lishe Endelevu Mkoa wa Morogoro, Nuhu Salehe , alisema mradi huo wa miaka minne ulizinduliwa kitaifa mwaka 2019 na unafadhiliwa USAID.

Chanzo: habarileo.co.tz