Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 14 tu ya Watanzania wana Bima ya Afya

NHIF TAZ Serikali yaruhusu kampuni binafsi kuuza mbolea

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: MillardAyo

Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu anayeshugulikia Afya OR-TAMISEMI, Dr. Grace Magembe imesema mpaka sasa Wananchi waliojiunga na Bima ya Afya Tanzania ni 14% tu huku 86% ya Watanzania wakiwa wanalipia huduma za matibabu kwa kutoa hela mfukoni pale wanapougua.

Dr. Grace amesema hii maana yake ni kwamba Watanzania wanapata changamoto pale ambapo wanapata maradhi na wakati huo hawana fedha mfukoni au hawapati huduma stahiki kwasababu hawana fedha ya kutosha kupata huduma hiyo kwa muda huo lakini pia Wananchi hao mara nyingi wanapata changamoto ya kuingia katika umasikini kwa sababu ya kugharamia matibabu kila wanapougua.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika Jijini Arusha Dkt. Grace amesema haijalishi unajiunga na Bima gani cha msingi kila Mwananchi awe na Bima ya Afya.

Dkt. Grace amesema tathmini ya haraka inaonesha Watu wengi hawana uelewa wa masuala ya Bima ya Afya lakini wengi wao wana uwezo wa kulipa na kufuatia hali hiyo amezitaka Kamati za Afya Mikoa na Wilaya(RHMT&CHMT) kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha katika kila ngazi ili kuwafikia Wananchi wengi zaidi kuhusu umuhimu wa kujiunga na Bima ya Afya.

Amesema Wananchi wakielimishwa vizuri watajiunga na Bima ya Afya yeyote ili kuondokana na adha wanayoipata pale wanapopata maradhi kwa kushindwa kugharamia matibabu na kusababisha madeni, umasikini na pengine vifo.

Chanzo: MillardAyo