Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 10 ya wanawake wanaotoa mimba kwa njia zisizo salama hufariki

Nyumba 52 Za Watumishi Zimejengwa Mwaka Huu Wa Fedha Dkt Mollel Naibu Waziri wa afya Dk. Godwin Mollel

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa afya Dk. Godwin Mollel amesema kuwa asilimia 10 ya wanawake wanaotoa mimba wanafariki kwa utoaji mimba usio salama.

Dk. Mollel ameyasema hayo leo wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu Conjesta Rwamlaza lililohoji kuhusu vifo vitokanavyo na utoaji mimba usio salama vina ukubwa na madhara gani.

Naibu Waziri Mollel amesema kuwa tafiti zilizofanywa zinaonesha matatizo yatokanayo na utoaji wa mimba ni moja ya sababu inayochangia vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 10.

Pia alihoji serikali imejipangaje kupunguza vifo vitokanavyo na utoaji mimba usio salama?

“Serikali mlisaini Mkataba wa Maputo ‘Maputo Protocol’ kutetea haki za wanawake na uzazi salama, makubalino hayo yalilenga mimba zitolewe zile za kubakwa, shambulio la ngono, mimba maharimu, serikali haioni umuhimu wa kuweka makubaliano hayo katika sheria za nchi yetu ili kuwasaidia wamama wanaopata mimba za namna hii waweze kuzitoa kwa usalama bila kuhatarisha maisha yao? alihoji Conjesta.

Amesema madhara yanayotokana na utoaji wa mimba usio salama ni pamoja na uambukizo mkali wa mfumo wa uzazi (Septic Abortion) ambao unaweza kupelekea mgonjwa kutolewa mfuko wa uzazi maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live