Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 10 ya Watanzania wanaviriba tumbo

56118 Pic+watoto

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali ya Tanzania iko mbioni kuajiri wahudumu wa afya wawili kila kijiji ambao pamoja na shughuli nyingine watatoa huduma za lishe kwenye ngazi ya kaya ili kupunguza matatizo ya afya yanayotokana na lishe duni, huku asilimia 10 ya Wanzania wakikabiliwa na tatizo la viriba tumbo linalotokana na hali hiyo.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Jumanne Mei 7 na Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustin Ndugulile ambaye amesema hadi sasa maofisa lishe 114 wameshaajiriwa katika mikoa na halmashauri.

Alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Zainab Mwamwindi ambaye alitaka kujua Serikali ina mpango gani unaotekelezeka wa kukabiliana na hali hiyo ikiwamo kuzijengea uwezo kamati za lishe za kata.

Naibu Waziri amesema Serikali ilianzisha huduma hiyo kwa kuwa na muundo wa kada ya maofisa lishe chini ya wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto mwaka 2012 ili kuboresha na kumaliza tatizo hilo kwa Watanzania.

Amesema kwa sasa Serikali inapitia sera ya taifa ya afya ya mwaka 2007 ikilenga kuboresha huduma za lishe kwa wananchi wake.

"Hata hivyo, Serikali imeongeza juhudi katika kupambana na tatizo la utapiamlo nchini kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi," amesema.

Habari zinazohusiana na hii

Hata hivyo, Dk Ndugulile amesema pamoja na juhudi za Serikali, Watanzania wanatakiwa kupunguza mlo usiokuwa na maana ili kupunguza viriba tumbo ambapo asilimia 10 ya Watanzania wanatajwa kuwa navyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz