Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apungua kilo 58 baada kuwekewa puto Mloganzila

Apungua Kilo 58 Baada Kuwekewa Puto Mloganzila Apungua kilo 58 baada kuwekewa puto Mloganzila

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Mkazi wa Ngara mkoani Kagera Bw. Charles Mwakameta amepungua kilo 58 baada ya kuwekewa puto maalum (intragastric ballon) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila na kukaa na puto hilo kwa takribani mwaka mmoja.

Bw. Mwakameta amepunguza uzito kutoka kilo 151 alizokuwanazo kabla ya Februari 20, 2023 alipowekewa putohadi kufikia kilo 92.65 alipotolewa puto hilo Februari 26, 2024.

Akielezea kuhusu safari yake ya kupungua uzito Bw. Mwakameta amesema ilianza baada ya kumuona msanii @peter_msechu ambaye aliwekewa puto hospitalini hapa na kuona kwamba huduma hii ni ya kweli na ina matokeo mazuri.

“Kipindi nilipokuja kuwekewa puto nilikuwa na kilo 151 lakini mpaka leo nimekuja kutoa puto baada ya mwaka mmoja nina kilo 92.65, watu walikua wakinicheka kutokana na uzito uliokithiri pia ninataka kuwaasa watanzania wenzangu wenye matatizo ya uzito mkubwa kuweka puto kunasaidia kupunguza uzito na wasiogope’’amefafanua Bw. Mwakameta.

Kufuatia matokeo hayo mazuri ameishauri kufika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila ili kupata huduma ya kuweka puto ambayo imemsaidia na hajapata madhara yoyote zaidi ameweza kubalilisha mfumo wake wa maisha.

Muhimbili Mloganzila ilianzisha huduma ya kupunguza uzito kwa kutumia puto (intragastric balloon) ambapo tangu kuanzishwa kwa huduma hii Novemba 2022 takribani wananchi 158 wamenufaika na huduma hiyo.

Chanzo: Bbc