Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila kwa kushirikiana na wale wa hospitali ya Muhimbili - Upanga wamemfanyia mgonjwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa saratani kwenye njia ya hewa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Masikio na Koo wa hosptali hiyo Raymond Leiya amesema upasuaji huo utasaidia saratani isisambae katika maeneo mbalimbali ya mwili wa mgonjwa na hivyo kutosababisha madhara zaidi.
Miongoni mwa visababishi vya saratani ya koo ni uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe uliopitiliza.
Dkt. Leiya ameishauri jamii kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa afya zao ili kuweza kubaini kama wana changamoto mbalimbali na hivyo kufanya matibabu mapema.