Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amref yawafikia wanafunzi wanafunzi 87,154

Bd394d3a819d41b865795b3c20a328e1 Amref Tanzania

Sat, 7 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Amref Tanzania limefanikiwa kuwafikia wanafunzi 87,154 kwa kugawa vifaa vya mbalimbali vya afya hasa vya kunawia mikono kwa lengo la kupambana na Convid 19 na magonjwa mengine ya kuambukizwa katika mikoa mitatu.

Wanafunzi hao pia wamefikiwa na mpango wa afya na mabadiriko ya Tabia kupitia mradi wa HBCC ambao umeanza kutekelezwa katika nchi za afrika miezi 12 iliyopita.

Mradi huo unaofadhiliwa na UKAID na Uniliver, ambao unajikita katika kuimarisha mabadiriko ya Tabia kwa wanafunzi katika kukabiliana na maeneo hatarishi ya umma tayari yametekelezwa katika shule za umma 64 na vituo vya kutolea huduma za Afya jijini Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Amref Tanzania Dk Florence Temu alisema mradi huu umelenga kuwalinda wanafunzi kujihusisha na Tabia Hatarishi zinazoweza kusababisha magonjwa yanayoambukiza kwa njia ya hewa kama COVID 19 shuleni hasa katika maeneo ya kufanya usafi.

"Lengo kuu la mradi huu ni mpango wa kutekeleza mabadiriko ya Tabia za ukuaji wa wanafunzi pamoja na kuwakinga na na magonjwa ya kuambukiza ndani ya maeneo ya mradi" Alisema Dk Temu.

Vifaa vya Afya ambavyo vimelenga kufikia mikoa mitatu iliyopo ndani ya mradi inalenga kuwahamasisha wanafunzi kunawa mikono hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana na magonjwa hatari ya mlipuko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live